The House of Favourite Newspapers

Sibomana: Lazima Niitungue Simba Leo Taifa

0
Patrick Sibomana.

MNYARWANDA Patrick Sibomana anayechezea Yanga, amesema atahakikisha anapambana kufa na kupona ili aifunge Simba, leo na kuweka rekodi. Tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi kuu, Sibomana ambaye amejiunga na Yanga msimu huu akitokea APR ya Rwanda amekuwa kwenye kiwango kizuri na mpaka sasa amefunga mabao manne na asisti moja.

Sasa leo atacheza Derby ya Kariakoo inayozihusisha Yanga na Simba pale Uwanja wa Taifa
kwa mara ya kwanza na anataka afunge ili aweke rekodi ya kufunga kwa mara ya kwanza dhidi ya wababe hao wa Msimbazi.

Sibomana ambaye amekuwa akiwavutia wadada wengi kutokana na muonekano wake ‘handsome’ aliliambia Championi Jumamosi kuwa, suala la kufunga ni la kila mtu kwenye timu na kwa upande wake huwa anapambana ili kuipa matokeo timu yake bila kujali nani atafunga.

 

Aliongeza kuwa katika mchezo wa leo atafanya jitihada kubwa ili aweze kufunga bao na kuisaidia timu yake iweze kupata pointi tatu muhimu na yeye kuweka rekodi yake.

 

“Nafikiri huu ni mchezo muhimu kwetu kupata pointi tatu, katika kila timu suala la kufunga ni jukumu la kila mchezaji, kikubwa ni kuhakikisha timu inapata matokeo.

 

“Pamoja na hayo kwa upande wangu nitapambana kwa nguvu ili niwafunge Simba na kuisaidia timu yangu kuondoka na pointi tatu muhimu na mimi kuweka rekodi ya kufunga katika mchezo mkubwa kama huo,” alisema Sibomana.

STORI NA Issa Liponda Dar es Salaam

Leave A Reply