The House of Favourite Newspapers

Siku 1, Watu 884 Wafariki kwa Corona Marekani, Vifo Vyafikia 5000

0

ZAIDI ya watu 5,000 wamefariki dunia nchini Marekani kwa sababu ya janga la Corona, ambapo zaidi ya watu 215,000 nchini humo wameambukizwa virusi hivyo, Chuo Kikuu cha Johns-Hopkins kimetangaza, shirika la habari la AFP limeandika.

 

Hii ni baada ya watu 884 kuripotiwa kufariki dunia katika saa 24, japo idadi hiyo ya Marekani ni ya chini ikilinganishwa na Italia na Hispania wakati huu maafa zaidi yakitarajiwa.

 

Wakati huohuo,  Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kwamba anatathmini uwezekano wa kusitisha safari za ndege za ndani katika miji ya Marekani iliyoathiriwa zaidi na janga la Covid-19 (Corona), jambo ambalo linaweza kuua watu wasiopungua 100,000 nchini humo, kulingana na ripoti ya mamlaka ya afya ya nchini Marekani.

 

“Tunatathmini hili, lakini mara tu hatua kama hiyo itakapochukuliwa, tutakuwa tumefunga sekta ambayo ni muhimu sana,”  amesema  Trump wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Ikulu ya White House.

 

Jumanne wiki hii  Trump alionya, siku mbili baada ya kuongeza hatua za kuangamiza janga la Corona hadi mwisho wa mwezi wa Aprili, kwamba wiki mbili “mbaya zaidi” zinatarajiwa kushuhudiwa nchini Marekani katika vita dhidi ya ugonjwa huo.

 

Leave A Reply