The House of Favourite Newspapers

Siku 26 Ngumu Yanga Kutamatika leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi

0
Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini.

NI kama zilikuwa siku ngumu kwa mashabiki wote wa Yanga baada ya kukaa muda mrefu bila kuishuhudia timu yao ikicheza katika ardhi ya Tanzania, jambo ambalo linatamatika rasmi leo Januari 30, 2024 watakapowavaa Hausing FC katika mchezo wa kombe la la Shirikisho la Azam Sports.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar ambapo utafanyika majira ya saa moja kamili usiku.

Yanga mara ya mwisho kucheza katika ardhi ya Tanzania ilikuwa ni Disemba 23, mwaka jana jambo ambalo linawafanya kuwa hawajacheza mechi yoyote tangia mwaka huu uanze.

Wananchi ambao mara ya mwisho kuiona Yanga ikicheza walikuwa ni Zanzibar katika michuano ya Mapinduzi Cup.

Katika mchezo huo wa mwisho kucheza ulikuwa ni mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United ambapo walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 liliofungwa na Clement Mzize huku asisti ikitolewa na Jesus Moloko ambaye kwa sasa sio mchezaji wa timu hiyo.

Katika hatua nyingine wananchi wamekaa siku 26 bila kuishuhudia timu yao ikiweza kucheza katika ardhi ya Tanzania.

UTATA! AVUNJIKA MGUU KIMAUZAUZA – ”MFUPA UMESIMAMA – MAUMIVU MAKALI – NAOGESHWA KWENYE KITI”…

Leave A Reply