The House of Favourite Newspapers

Video: Mama Nandy Afunguka Baada Ya Kumzika Mwanaye Aliyeuawa Kinyama Na Wanaodaiwa Kuwa Sungusungu….

0


Mama wa kijana anayedaiwa kuuawa na sungusungu anayejulikana kwa jina maarufu la Mama Nandy, amezungumza tena na Global TV baada ya kumaliza shughuli ya kumzika kijana wake ambapo ameomba mamlaka zinazohusika, kutenda haki juu ya kifo cha mwanaye.

Mwanamke huyo, mkazi wa Yombo jijini Dar es Salaam amesema kwa kipindi chote cha msiba wa mwanaye, hakupata ushirikiano wowote kutoka Serikali ya Mtaa ambayo ndiyo inayowasimamia sungusungu hao.

Siku ya tukio, inaelezwa kuwa kijana huyo aliyekuwa na changamoto ya afya ya akili, alitoka usiku kwenda kuchota maji, ambapo alikutana na sungusungu ambao baada ya kushindwa kuelewana, walianza kumpiga na kusababisha kifo chake.

Leave A Reply