The House of Favourite Newspapers

Siku Ya Mazingira Duniani: Exim Yakabidhi Vifaa vya Usafi Dar

0
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania Bw Stanley Kafu (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija (katikati) vifaa vya usafi vilivyotolewa na benki hiyo ili kuimarisha hali ya usafi katika jiji la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake kinatarajiwa kuwa Juni 5 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bi Charangwa Makwiro (wa tatu kushoto) na pamoja na wafanyakazi wa Exim Bank.

Benki ya Exim imekabidhi vifaa vya usafi kwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake kinatarajiwa kuwa Juni 5 mwaka huu.

 

Hatua hiyo ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo wa kutunza mazingira unaofahamika kama Exim Go Green Initiative.

 

Akipokea msaada huo jijini Dar es Salaam  mapema hii leo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa msaada huo.

 

Alitumia fursa hiyo kuzialika taasisi mbalimbali kushiriki kwenye utunzaji wa maeneo ya asili ikiwemo fukwe za bahari, kupanda miti na maua kwenye maeneo ya wazi na hifadhi za barabara pamoja kuhifadhi  bustani zilizopo maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

 

“Jitihada kama hizi zinazooneshwa na benki ya Exim sambamba na shughuli nyingine nyingi  zitaendelea wiki nzima kuanzia Juni mosi hadi Juni 5 ambayo ndio siku ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira.” Alibainisha  Bw Ng’wilabuzu na kuwahimiza wakandarasi wanaotoa huduma ya uzoaji taka katika jiji hilo kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya kutosha na kutoa huduma  inayokidhi mahitaji ya wananchi kwa wakati.

Alisema maadhimisho hayo  yataambatana na shughuli mbalimbali inayolenga kuongeza hamasa za utunzaji wa mazingira ikiwemo mikutano ya Kitaaluma juu ya masuala ya mazingira, matamasha ya maonyesho, kampeni za usafi wa mazingira, shughuli ambazo zitaendelea kwa wiki nzima kuanzia Juni mosi.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim, Bw Stanley Kafu  alisema msaada huo unahusisha vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi ikiwemo matoroli ya kubebea takataka, vyombo vya kuhifadhi takataka,  mafagio, reki pamoja na makoleo.

 

“Siku ya Mazingira Duniani ni siku ambayo inahitaji jitihada za pamoja  ili kuhakikisha suala zima la usafi na muonekano wa mazingira linapatiwa ufumbuzi. Hiyo ndio sababu benki ya Exim tunaamini  sana umuhimu wa kusaidia mipango ya mazingira ambayo ina faida za moja kwa moja kwa jamii. ’’ alisema Bw Kafu.

Mbali na kuongoza kampeni mbalimbali za upandaji miti ikiwemo  ile ya upandaji miti 10,0000 iliyofanyika hivi karibuni jijini Dodoma kwa ushirikiano  na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, benki hiyo pia imekuwa imekuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa bustani mbalimbali zilizopo kwenye baadhi ya majiji hapa nchini ikiwemo Dar es salaam.

Leave A Reply