The House of Favourite Newspapers

Bata la Nandy Hatari – Video

0

Usiku wa kuamkia leo, malkia wa Bongo Fleva, officialnandy amekutanisha baadhi ya wasanii wenzake na kuwapa bata la hatari.

 

Ishu hiyo imejiri kwenye kambi aliyoweka Nandy au The African Princes kwenye nyumba moja pande za Masaki jijini Dar iliyopewa jina la Nandy Festival House 2021.

 

Baadhi ya mastaa waliohudhuria ni wale watakaokuwa kwenye ziara ya Nandy Festival ambao itaanza hivi karibuni.

 

Baadhi yao ni @officialbabalevo, @dullamakabila, @mabantuofficial na wengine ambapo mbali na kula na kunywa hadi kusaza, pia kila mmoja alipewa chumba cha kulala na kujiachia kwa raha zao.

CC: @sifaelpaul

 

 

Leave A Reply