The House of Favourite Newspapers

Simalenga Akunwa Na Jitihada Za Kilimanjaro One Kukuza Utalii Wa Kiutamaduni Bariadi

0
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mh. Simon Simalenga (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Kilimanjaro One Travel and Tours walipokutana katika ofisi ya mkuu wa mkoa ili kufanya mazungumzo kuhusu tamasha la Lake Zone Cultural and Tourism Festival linalotarajiwa kufanyika Bariadi mwezi Julai.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mh. Simon Simalenga amaipongeza kampuni ya Kilimanjaro one Travel and Tours kkwa kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali katika kukuza utalii wa kiutamaduni.

Mkuu huyo wa Wilaya aliyasema hayo ofisini kwake  wakati akifanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa kampuni ya Kilimanjaro One waliomtembelea ofisini kwake kufanya mazungumzo kuhusu tamasha la Lake Zone Cultural and Tourism Festival ambalo litafanyika Bariadi Simiyu July 5, 6 na kilele chake ni July 7, 2024.

“Tamasha hili linaendana na azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kila halmashauri  inaandaa tamasha la utamaduni na utalii,” alisema.

Mh. Simalenga alisema serikali iko tayari kutoa ushirikiano kwa waandaaji hao na kuwalumbusha kuwa wasukuma wanathamnini utamaduni wao na huwa wako tayari kuutangaza  muda wote.

“Tunataka wageni waje kwa wingi wahionee utamaduni wa wasukuma na tunaamini kuwa jambo hili litawavutia watu wengi zaidi  kwani mkoa wetu wa Simiyu una vivution vingi vya kitamaduni na kitalii.

Pia, alitoa wito kwa mashirika mbalimbali ya uma nay a binafsi inayofanya shughuli zake katika eneo hilo kuhakikisha yanadhamini tamasha hilo ambalo litaenda sambamba na maonyesho ambayo yatawapa wadhamini nafasi ya kujitangaza bidhaa na huduma zao.

Alitoa wito kwa waandaaji hao pia wahakikishe wanatangaza tamasha hilo kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari na magari ya matangazo ili ujumbe ufike kwa watu wengi zaidi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kilimanjaro One Travel and Tours, Mohamed Hatibu alisema kampuni yake imejiandaa vizuri kuratibu tamasha hilo ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza lakini litakuwa inafanyika kila mwaka katika Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu.

“Tunatarajia kukusanya watu wasiopungua 7,000 katika tamasha hili maarufu kama mbina ambalo huwa ni hafla maalumu kuadhimisha kilele cha msimu wa mavuno katika jamii ya wasukuma.

Alisema tamasha hilo pia lina lengo la kuwavutia watalii wa ndani na nje na kusisitiza kuwa I muda mwafaka sasa kuutangaza utamaduni wa Simiyu ili dunia nzima ifahamu,” alisema.

Alimueleza Mkuu wa Wilaya kuwa mipango inaendelea vizuti ili kuhakikisha tamasha hilo linafanyika kwa kiwangi cha hali ya juu mna kuongeza kuwa hakutakuwa na kiingilio kwa watu wote watakaopata fursa ya kujionea matukio mbalimbali katika tamasha hilo.

Leave A Reply