The House of Favourite Newspapers

Simanzi: Mwili wa Isaac Gamba Wawasili Mwanza – Pichaz

MWILI wa aliyekuwa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) nchini Ujerumani, Isaac Muyenjwa Gamba umewasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza leo Jumanne, Oktoba 30, 2018 asubuhi ukitokea jijini Dar es Salaam ambako uliagwa jana.

Sudi Mnete ( wa pili kulia) akiwa na waombolezaji wengine uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Baada ya kuwasili Mwanza, mwili huo umepelekwa katika Viwanja vya UTPC jijini humo kwa ajili ya  ibada fupi na kuaga kabla ya kuelekea nyumbani kwao Bunda mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.

Marehemu  hakuwahi kuugua ugonjwa wowote wa kuaminika zaidi ya kukutwa akiwa amefariki chumbani kwake Alhamisi, Oktoba 18, mwaka huu, jijini Bonn nchini Ujerumani alikokuwa akifanya kazi zake.

Baada ya uchunguzi wa hospitali nchini Ujerumani, imegundulika kuwa kilichosababisha kifo chake ni kuvuja kwa damu kwenye ubongo (Brain Hemorrhage) yaani presha ya damu.

SIMANZI! MWILI WA ISAAC GAMBA UKIAGWA LUGALO – VIDEO

PICHA NA DENIS MTIMA | GPL

Comments are closed.