The House of Favourite Newspapers

Simba Azam Moyo Sukuma Damu

azam-na-simba-1Na Ojuku Abraham | GAZETI LA IJUMAA

KIBAO kipya cha msanii Lameck Ditto anayefahamika zaidi kama Ditto, ambaye yupo katika Jumba la Kukuza Vipaji (THT) kiitwacho Moyo Sukuma Damu, ndiyo habari ya mjini kwa sasa.

Na ameweka wazi kabisa, kuwa kazi hasa ya moyo ni kusukuma damu ili isambae katika mfumo wa mwili wa binadamu. Lakini binadamu wameupa moyo kazi nyingi zaidi.

omogKocha wa Simba , Joseph Omog akiwafua viajana wake.

Kuna ambao wameupa moyo kazi ya kupenda wenzao na kwa matamanio yao ya kibinadamu, wanaulazimisha wakati mwingine unafanya kazi kwa haraka kuliko uhalisia wake.

Na hii ndiyo kazi ambayo Simba na Azam inawapa wachezaji, viongozi na mashabiki wake, wakati kesho zitakapokutana katika Uwanja wa Uhuru kuwania pointi tatu za Ligi Kuu Bara.

ciobaKocha mpya wa Azam, Mromania, Aristica Cioaba.

Timu hizo zinakutana zikiwa ni takribani siku 15 zimepita tangu mara ya mwisho zikutane katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi kule Zanzibar, ambapo Simba walilala kwa bao 1-0.

Mioyo ya mashabiki wa pande zote mbili itakuwa ikidunda kwa kasi zaidi muda wote wa mchezo hali ambayo kwa mtu asiyekuwa mvumilivu anaweza kupatwa na shinikizo la damu.

john-boko

John Boko ‘Adebayor’

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Simba ambao ni wakongwe zaidi katika soka kuliko Azam, waliibuka na ushindi wa bao 1-0. Simba kwa sasa wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 45 ambazo ni 14 zaidi ya Azam inayoshika nafasi ya nne baada ya zote kucheza mechi 19. Ni mchezo wa presha kwa sababu timu hizo zote zinahitaji pointi tatu kwani endapo moja ikitokea imeteleza, basi itakuwa imepoteza matumaini ya kufikia malengo yao.

Simba wako mbele ya Yanga kwa pointi mbili, hivyo kitendo cha wao kupoteza pointi tatu kutatoa nafasi kwa mabingwa hao watetezi kuipoka nafasi ya kwanza kama na wao watashinda dhidi ya Mwadui, Jumapili hii.

azam-vs-simba_nsvtm3ugt43k191l1ftwpdoo4Azam licha ya kuinyuka Simba kwenye Mapinduzi, imekuwa haina matokeo mazuri katika ligi, hivyo itawalazimu kujituma zaidi kuhakikisha wanarudisha makali yao kama ilivyokuwa misimu ya nyuma.

Wachezaji wao mahiri Himid Mao, John Bocco ‘Adebayor’, Joseph Mahundi na wengine, watakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha wanapata ushindi wao wa kwanza katika ligi wakiwa chini ya kocha wao mpya, Mromania, Aristica Cioaba.

ijumaa1Gazeti la Ijumaa

Mromania huyo ambaye alikuwa hajaanza kazi kutokana na kukosa kibali cha kufanyia kazi nchini, kesho anaweza kukaa katika benchi kutokana na suala lake hilo kuonekana kukamilika kwa kiasi kikubwa. Hii ni moja ya mechi ngumu zaidi ambazo timu hizo zinakutana kila msimu na ugumu wake unatokana na uimara wa vikosi vyote viwili.

Mchezo baina ya timu hizi hautabiriki na yoyote anaweza kukalishwa, kwani hakuna kikosi chenye njaa. Kama nilivyosema hapo mwanzo, kazi ya moyo ni kusukuma damu, hakuna sababu ya mashabiki kujipa presha wakati inaeleweka yeyote kati yao anaweza kushinda, kufungwa au kutoshana nguvu kwa sababu mchezo wa soka una matokeo matatu.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.