The House of Favourite Newspapers

Simba Bingwa Kombe la FA, Yaipiga Namungo 2-1

0

TIMU ya Simba leo Agosti 2, 2020 imerejea kile ilichokifanya msimu wa mwaka 2016/17 baada ya kushinda mabao 2-1 mbele ya Mbao FC iliyokuwa imepanda Ligi Kuu msimu huo.

Simba imevuna tena ushindi wa namna hiyo kwa Namungo FC ambayo ni msimu wake wa kwanza kushiriki Ligi Kuu na kutinga hadi fainali ya Kombel la Azam Sports Federation (ASFC) katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Simba ndio ilikuwa ya kwanza kufumania nyavu za wapinzani baada ya bao la Luis Miquissone dakika ya 27 huku bao lao la pili likifungwa na John Bocco dakika ya 39.

Mabao hayo yaliwaweka Simba kifua mbele hadi dakika ya 56 Edward Manyama alipofunga bao moja kwa Namungo na kuwarejesha mchezoni.

Miquissone alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa fainali na kujinyakulia Sh 500,000.

Leave A Reply