The House of Favourite Newspapers

Simba Kupata Ushindi wa Mezani Dhidi ya Al Merrikh

0

KLABU ya Simba huenda ikapata ushindi wa mezani dhidi ya Al Merrikh kutokana na timu hiyo ya Sudan kudaiwa kuwatumia wachezaji wawili ambao hawakupaswa kucheza katika mchezo baina yao uliochezwa jijini Khartoum, Jumamosi iliopita ambao uliisha kwa sare tasa.

 

Taarifa za uhakika ambazo uongozi wa Simba umedai kuzinasa kutoka Sudan kwa ushahidi wa nyaraka mbalimbali, zimeonyesha kuwa wachezaji hao Ramadan Agab, Mohamed Bakhit Mahmoud Mohamed, walicheza mechi hiyo huku wakiwa wanatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita waliyopewa na Chama cha Soka Sudan (SFA).

 

Ushahidi wa barua ambao Simba wameupata  unaonyesha kuwa SFA iliwafungia wachezaji hao kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kusaini mikataba katika timu mbili tofauti, adhabu ambayo inaishia katikati ya Aprili.

 

Wachezaji hao hawakucheza mechi yoyote ya Al Merrikh hadi sasa wamefungiwa kucheza hadi katikati ya Aprili, wamefanya uamuzi wao wenyewe,” alisema mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.

 

Ikiwa itabainika ni kweli Al Merrikh waliwachezesha wachezaji ambao hawakustahili kucheza, itaondolewa mashindanoni.

Leave A Reply