The House of Favourite Newspapers

Simba na Al Ahly Zatunishiana Sauzi

SIMBA imeingia kwenye mpambano mkubwa wa kimilionea wa kusaka saini ya straika wa Orlando Pirates, Justin Shonga. Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, wameripotiwa kuwania mchezaji huyo sambamba na klabu zenye msuli mkubwa wa kifedha ambazo ni Eibar ya Hispania na Al Ahly ya Misri.

 

Mchezaji huyo wa Zambia, amepachika mabao 13 kwenye mashindano yote msimu uliopita lakini inadaiwa kwamba alikomea hapo kutokana na majeruhi jambo ambalo wanaojua soka wanaamini msimu huu ataibuka kibabe. Kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini mchezaji huyo aliibeba klabu yake licha ya kupachika mabao sita.

 

Mabao matatu ya Shonga kwenye mashindano yote yalifungwa kwa mipira ya adhabu na alikuwa na asisti saba ambapo inadaiwa kwamba klabu yake ina mpango wa kumbakisha kwavile ni miongoni mwa wachezaji wenye
uzoefu mkubwa ndani na nje ya Uwanja.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Cresentius Magori alisisitiza juzi kwamba Simba imebakiza nafasi moja na mchezaji huyo wanayemalizana naye ataibuka kambini hapa Sauzi.

 

Licha ya kwamba Magori na vigogo wenzie kufanya siri, lakini Spoti Xtra linajua kwamba Shonga yupo kwenye rada yao na wamezungumza naye mara kadhaa ingawa mchezaji huyo hajafanya maamuzi ya mwisho. Orlando wanamshawishi kwa nguvu zote asalie.

Comments are closed.