The House of Favourite Newspapers

Simba Queens na JKT Queens Vita ya Mashujaa

Wachezaji wa timu ya Simba Simba Queens 

LEO Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League inaendelea ambapo vita kubwa inatarajiwa kuwa kati ya mchezo wa Simba Queens na JKT Queens mchezo utakaochezwa Uwanja wa Karume.


Rekodi zinaonyesha katika timu 12 ambazo ni moto wa kuotea mbali kwa sasa kati ya zinazoshiriki Ligi ya wanawake huwezi kuiacha JKT Queens ambayo katika michezo mitano waliyoshuka Uwanjani hawajapoteza hata mchezo mmoja wakiwa na pointi 15 wakiwa nafasi ya kwanza.

Wapinzani wao Simba Queens wao wamepata sare mchezo mmoja wakiwa na pointi 13 kwenye msimamo wakiwa nafasi ya pili hivyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa unawakutanisha mashujaa wawili.

Timu nyingine ambazo zitashuka Uwanjani leo ni pamoja na Alliance Girls dhidi ya Marsh Queens Uwanja wa Nyamagana, Tanzanite SC dhidi ya Evergreen Uwanja wa Amri Abeid, Baobab Queens dhidi ya Yanga Princess Uwanja wa Maj.Gen.Isamuhyo.

Mapinduzi Queens wao wataikaribisha Sisterz FC Uwanja wa Sabasaba na Mlandizi Queens wao watamenyana na Panama FC Uwanja wa Mabatini. Michezo yote itachezwa leo saa 10 Jioni.

Comments are closed.