The House of Favourite Newspapers

Kagere Atoa Kauli Nzito Kwa AS Vita

Meddie Kagere

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, amesema wanakwenda DR Congo kupambana na hawataingia kinyonge.

Kagere ametoa kauli hiyo wakati Simba, kesho Alhamisi ikitarajiwa kwenda DR Congo kucheza dhidi ya AS Vita mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

 

Katika mchezo uliopita dhidi ya JS Saoura, Kagere alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 3-0. Mchezo huo ulichezwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 

“Mechi ya ugenini si sawa na nyumbani, tunajua wapinzani wetu watakuwa wamejipanga kwelikweli, lakini hatutakuwa wanyonge.

 

“Tutapambana nao kwa vyovyote vile, lengo ni kupata pointi tatu kwao na kujipanga na mchezo mwingine,” alisema Kagere.

Comments are closed.