The House of Favourite Newspapers

SIMBA RAMADHAN AJINYAKULIA PIKIPIKI MPYA TUSUA MAISHA NA GLOBAL

Wakati washindi wa droo ya saba na nane wa Shindano la Tusua Maisha na Global wakitarajiwa kukabidhiwa zawadi zao, Ijumaa Agosti 24, 2018, Simba Ramadhan, mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam ameibuka mshindi wa kwanza katika droo ya tisa na kujishindia pikipiki mpya.

 

“Kwa kweli wakati napigiwa simu sikuamini, namshukuru sana Mungu na ninasema Alhamdulilah kwa hii zawadi niliyoipata. Unajua mimi ni dereva wa magari yote lakini kwa muda mrefu sijapata ajira kwa hiyo nilikuwa nafanya shughuli zangu za ujasiriamali kwa hiyo Global ni kama wameniona.

 

“Kwa miaka mingi mimi ni msomaji mkubwa wa magazeti ya Ijumaa na Ijumaa Wikienda, yaani niko radhi hata nisile lakini siyo kuyakosa magazeti haya, wakati mwingine mpaka nikawa nagombana na mke wangu lakini Alhamdulilah leo nimeyaona matokeo ya kusoma magazeti ya Global,” alisema Simba kwa furaha kubwa.

 

Wengine waliong’ara katika droo ya tisa ni Anna Mbise, mfanyabiashara kutoka Arusha aliyejishindia dinner set na Hussein Mtipa wa Ifakara, Morogoro aliyejishindia jezi.

 

Wanaotarajiwa kukabidhiwa zawadi zao Ijumaa ni Said Katambo wa Nachingwea, Lindi na Jackson Bwire wa Ukerewe, Mwanza waliojishindia pikipiki, Nobert Benjamin wa Nyamagana Mwanza na Boniface Malick wa Bunju A jijini Dar es Salaam waliojishindia dinner set.

 

Wengine ni Benard Kasembe wa Pugu Mwakanga aliyejishindia head phones za kisasa za Beats by Dre, Gasper Ndimbo, mkazi wa Miseko, Mkuranga na Ally Bakari, Mkazi wa Vikindu waliojishindia jezi.

 

Wakati huohuo, washindi wa droo ya tisa, wamepatikana katika droo iliyochezeshwa Jumanne ya Agosti 21, 2018 na kurushwa mubashara kupitia Global TV Online ambapo majina ya washindi na zawadi zao kwenye mabano ni Simba Ramadhan, mkazi wa Mbezi aliyejishindia pikipiki, Anna Mbise wa Arusha aliyejishindia dinner set na Hussein Mtipa wa Ifakara, Morogoro aliyejishindia jezi.

 

Ili kuwa miongoni mwa washindi, nunua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers kati ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra kisha funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki.

 

Itume namba maalumu inayoonekana juu ya kuponi kwa njia ya meseji kwenda namba 0719386533. Hakikisha unahifadhi kuponi au gazeti lako kwani linahitajika wakati wa kuchukulia zawadi vigezo na masharti vinazigatiwa.

 

Comments are closed.