SIMBA SC ITAUZA WENGI SANA ULAYA

Emmanuel Okwi (kushoto) akiwa na Claytus Chama

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kama wachezaji wake wataendelea kucheza kwa kiwango cha juu katika michuano ya kimataifa ni wazi sio Emmanuel Okwi au Claytus Chama watapata ofa za maana pekee bali mastaa kibao.

 

Habari zilizopo ni kwamba Okwi anakwenda Kaizer Chief ya Afrika Kusini huku Chama akipata ofa Uturuki na Kuwait.

Akizungumza na Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili, Aussems alisema; “Unajua tumecheza mechi zile za awali za kimataifa tayari wachezaji wangu nasikia wanatakiwa na timu za nje ingawa suala hilo halijafika mezani nasikia tu lakini ukweli wachezaji wangu wapo vizuri hilo najivunia.

 

“Na hivi tunaenda kukutana na Nkana (ya Zambia) kama wataendelea kupambana kwa nguvu na bidii mwisho wa siku wakapata matokeo basi ni wachezaji wengi wa timu yangu watahitajika nje kutokana na viwango ambavyo wanaonyesha kwa sasa.”

 

Kwa upande mwingine kocha huyo amefunguka kuwa: “Nimeona baadhi ya mechi za Nkana lakini zilikuwa za nyuma kidogo ninaamini zitakuwa msaada kwetu lengo ni kwenda kufanya vyema kuhakikisha tunapata matokeo tukiwa ugenini.”

Loading...

Toa comment