The House of Favourite Newspapers

Simba SC tulieni, John Bocco atawavaa Waarabu

MSHAMBULIAJI wa Simba, John Bocco sasa amerejea rasmi na atacheza mechi dhidi ya Al Ahly itakayopigwa Februari 2, mwaka huu nchini Misri.

 

Bocco aliumia kifundo cha mguu kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura na kusababisha akose mechi dhidi ya AS Vital ya DR Congo ambayo Simba ililala mabao 5-0.

 

Simba imepanga kuwafuata Al Ahly keshokutwa Jumatatu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo. Kocha wa Simba, Patrick Aussems ameliambia Championi Jumamosi kuwa: “Mshambuliaji wetu John Bocco anaendelea vizuri na mechi yetu ijayo dhidi ya Al Ahly katika Ligi ya Mabingwa Afrika anaweza kucheza.

Na Khadija Mngwai

Comments are closed.