The House of Favourite Newspapers

Kikosi cha Simba Kimetamba Kushiriki Hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho

0
            Kikosi cha Simba kinachoshiriki robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika

UONGOZI wa kikosi cha Simba, umetamba kuwa walikuwa tayari wamejiandaa kukutana na mpinzani yeyote kwenye Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na wanaamini wana uwezo wa kuwaondoa Orlando Pirates ya Afrika Kusini na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

 

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika Simba wamefuzu hatua ya robo fainali baada ya Jumapili iliyopita kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya timu ya USGN ya Niger kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

 

Katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba wamepangwa kuvaana na wababe wa soka la Afrika Kusini Orlando Pirates, ambapo Simba wataanzia nyumbani Aprili 17, mwaka huu kabla ya kwenda kumalizia ugenini Aprili 24, mwaka huu.

          Bernard Morrison akiwa katika harakati uwanjani

Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema: “Ni wazi kuwa tumepangwa dhidi ya wapinzani wagumu, kila mtu anaujua ukubwa wa jina la Orlando Pirates kwenye soka la Afrika kutokana na rekodi ambazo wamefanikiwa kuziweka, lakini mpaka Simba imefikia hatua hii basi ni uthibitisho tosha wa ukubwa wetu.

 

“Tutaanzia nyumbani na niweke wazi kuwa tulikuwa tayari kukutana na timu yoyote, tumejipanga vizuri kutumia faida ya uwanja wa nyumbani kupata matokeo, kwetu lazima tupate matokeo hapa nyumbani na kwenda kupambana ugenini, tunaamini kuwa tutawatoa Orlando na kucheza nusu fainali.”

Leave A Reply