The House of Favourite Newspapers

Nandy: Nitakufa Lakini Lazima Niwasadie Wasichana Wanaopitia Changamoyo

0
Faustina Charles Mfinanga almaarufu Nandy.

Faustina Charles Mfinanga almaarufu Nandy; ni malkia wa muziki Afrika Mashariki ambaye anasema kuwa, umaarufu wake hauwezi kuwa na maana hata kidogo kama hawezi kuutumia hata nusu kwa aliji ya jamii yake kwa sababu hautakuwa na maana kabisa kwake na hata jamii inayomzunguka.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Nandy au Nandera anasema kuwa, alikuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuwasaidia wasichana wanaopitia changamoyo mbalimbali hivyo akaona kabla siku yake ya kufa haijaifika, awe ameshafanya mambo kadhaa kwa jamii yake kupitia kampeni yake ya Funguka Kampeni ili aweze kuacha alama kwa jamii yake.

 

“Kuacha alama kwenye jamii ni kitu kizuri sana na ninachokiomba kabla ya kufa nifanye mambo niliyojipangia kuhusu jamii yangu kama kusaidia wasichana wadogo waliokata tamaa ya kusoma kutokana na changamoto mbalimbali na hata nikifanya mambo niliyoyaasisi, lazima yaendelee kufanyika,” Nandy.

Stori; Imelda Mtema, Dar

SIMBA KWENYE NYIMBO ZA UBINGWA WAPO, AGREY AUKUBALI MZIKI WA MAYELE | KROSI DONGO

Leave A Reply