The House of Favourite Newspapers

Simba: Ubingwa Mapema Tu, Prisons Wanakufa

0

BENCHI la ufundi la Klabu ya Simba limefunguka kuwa, linawaandaa wachezaji wake kuwa fiti kimwili na kiakili kuhakikisha wanafanikiwa kutwaa pointi tatu za Tanzania Prisons ili kutwaa ubingwa wa msimu huu 2019/20.

 

Simba inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa na pointi 78, itashuka dimbani keshokutwa Jumapili kumenyana na Tanzania Prisons mchezo ambao watatangazia ubingwa iwapo watashinda.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alifunguka kuwa, kocha Sven anawaandaa vyema wachezaji wake kisaikolojia ili kuwaweka fiti kabla ya kukutana na Prisons kuhakikisha wanaibuka na pointi tatu muhimu.

 

“Kwa tunachokiangalia hapa ni kuona ni jinsi gani kikosi chetu tunakiandaa kuelekea mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons, tuweze kupata ushindi ndipo tusherehekee ubingwa.

“Mwalimu anaendelea na program zake za mazoezi kama kawaida kwa kuwaweka fiti wachezaji katika mazoezi ikiwa ni pamoja na kuwaweka sawa kisaikolojia ili kuhakikisha tunafanikiwa kuibuka na pointi tatu muhimu.

 

“Kikosi chetu kipo vizuri, hatuna majeruhi hata mmoja, majeruhi ambaye alikuwepo Mkude (Jonas) sasa anaendelea na mazoezi ya pamoja na wachezaji wengine, mwalimu anajaribu kuwaweka sawa wachezaji wote katika utimamu wa kimwili kati ya wale waliocheza dhidi ya Mbeya City na wale wasiocheza ili wote waweze kuwa sawa tayari kwa mechi,” alisema Rweyemamu.

Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Leave A Reply