The House of Favourite Newspapers

Simba vs Mtibwa Kazi Ipo leo Jumapili Uwanja wa Mkapa, Dar… Kocha Mgunda Afunguka

0
Kikosi cha timu ya Simba.

ITAKUWA kazi kubwa ndani ya dakika 90 leo Jumapili Uwanja wa Mkapa, Dar, ambapo Simba itawakaribisha Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, huku kila timu ikibainisha kuwa inahitaji pointi tatu.

 

Kwa namna hiyo, inaamanisha kwamba acha inyeshe tuone panapovuja kwa wababe hawa wawili watakaokuwa kwenye msako wa pointi tatu.

 

Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba, alisema: “Tumetoka kupoteza mchezo dhidi ya Azam FC, kwa sasa tupo tayari kwa mchezo dhidi Mtibwa Sugar, wachezaji wote wapo tayari.

 

“Kuhusu Erasto Nyoni, ni mchezaji wa Simba na anastahili kutimiza majukumu ya Simba muda wote, wachezaji wote waliosajiliwa kazi yao ni moja, kutafuta ushindi.

 

“Kwa sasa idadi ya majeruhi inapungua ambapo Nelson Okwa na Jimmyson Mwanuke ambao hawapo vizuri, lakini wengine waliobaki wote wapo tayari.

Wachezaji wa timu ya Mtibwa.

“Kushinda au kwenda sare ni matokeo ya mchezo, katika kupoteza ni sehemu ya mchezo pia, hivyo kuna mazuri ambayo tuliyafanya, yale mapungufu tumeyaona na tumeyafanyia kazi.”

 

Nahodha Msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein, alisema: “Kupoteza ni sehemu ya mchezo na Simba ni timu kubwa, tumeanza kurejea katika ubora.

 

Matokeo yaliwaumiza wengi lakini sisi bado ni bora, Wanasimba wajitokeze kutushangilia.” Awadhi Juma, Kocha Msaidizi wa Mtibwa Sugar, alisema: “Tunakwenda kukutana na timu ngumu ambayo imetoka kupoteza, lakini tunawaheshimu wapinzani wetu, tunaamini tutapata matokeo mazuri.

 

“Tumekuwa tukitengeneza nafasi na kushindwa kuzitumia, Charles Ilanfya ni miongoni mwa washambuliaji wazuri, hakukosa nafasi dhidi ya Yanga tu, bali kuna mechi nyingine alikosa, lakini ana mabao matatu, pia anatoa pasi za mabao, tunaamini akiamka salama kesho (Leo) anaweza kufunga.”

 

George Chota, nyota wa Mtibwa Sugar, alisema: “Nafasi ambayo tupo inatupa presha ya kuendelea kutafuta matokeo mazuri, unajua kwamba Mtibwa Sugar ni chuo, hivyo tunakwenda kutoa burudani.”

WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

UTAMU MCHUNGU wa MITANDAO ya KIJAMII, JOYCE KIRIA, WANASHERIA WAFUNGUKA | MAPITO..

Leave A Reply