The House of Favourite Newspapers

Simba Waifuata ASEC Mimosas usiku, Ayob Lakred, Onana Out

0

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa maandalizi kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas yapo vizuri na kikosi kimekwea pipa kueleka Ivory Coast leo Februari 20.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Februari 23 ikiwa ni hatua ya makundi ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 1-1 ASEC Mimosas.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua ugumu wa mchezo huo na maandalizi yanafanyika kwa ukamilifu ili kupata matokeo mazuri.


“Alfajiri ya Jumanne kikosi kinaanza safari kutoka Tanzania kuelekea Ivory Coast, tunamshukuru Mungu wachezaji wamepata muda mwingi wa kufanya mazoezi na maandalizi mazuri kwenye mchezo huo.
“Mazoezi ya Jumatatu ni ya mwisho kwetu hapa Dar na usiku tunaanza safari kuelekea Ivory Coast tukipitia Ethiopia. Unaweza kuona tunakabiliwa na safari ya saa nyingi na jopo la kwanza limetangulia Ivory Coast kuandaa taratibu zote.
“Mratibu Abbas Ally yeye alitangulia na tunatarajia kuondoka na wachezaji 23 huku Ayoub Lakred akikosekana kwa kuwa ana kadi tatu za njano, Willy Onana anasumbuliwa na nyama za paja,” .

Leave A Reply