The House of Favourite Newspapers

Simba wasepa zao Zenji Kucheza Dhidi ya Kipanga FC ya Unguja, Zanzibar

0
Wachezaji wa timu ya Simba.

KATIKA kuhakikisha anatengeneza muunganiko wa kikosi imara cha Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda, ameomba michezo miwili ya kirafiki ambayo watacheza dhidi ya Kipanga FC ya Unguja, Zanzibar.

 

Kipanga wiki iliyopita ilifanikiwa kufuzu hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwafunga Al Hilal Wau FC ya nchini Sudan.

 

Simba ipo katika maandalizi ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Clube De Desportivo de Agosto ya nchini Angola.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa kikosi chao kitaondoka jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa kuelekea Zanzibar tayari kwa ajili ya mchezo huo.

 

Ally alisema kuwa wanakwenda kucheza mchezo mara baada ya kupokea mwaliko waliopewa na Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF) ambapo watacheza michezo miwili ya kirafiki.

 

Aliongeza kuwa mchezo wa kwanza watacheza Septemba 25, mwaka huu dhidi ya Kipanga ambao utapigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

 

“Mchezo wa kwanza utakuwa keshokutwa Jumapili na siku mbili mbele wataucheza mwingine kwenye uwanja huo wa Amaan ambapo mechi zote zitachezwa saa moja usiku.

 

“Baada ya michezo hiyo miwili timu itarejea Dar es Salaam Septemba 28, mwaka huu tayari kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Agosto,” alisema Ally.

STORI; WILBERT MOLANDI

MORRISON AANZA BALAA, AFUNGIWA MECHI TATU, CEO SIMBA APATA SHAVU CAF | KROSI DONGO

Leave A Reply