The House of Favourite Newspapers

Simba Watamba kuanza kupata ushindi dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco

0

BAADA ya kukosa ushindi katika michezo miwili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imepanga kuanza kupata ushindi dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.

Simba imevuna pointi mbili pekee ikicheza michezo miwili ya Kundi B katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Timu hiyo, itakuwa na kibarua kingine keshokutwa Jumamosi watakapocheza dhidi ya Wydad Casablanca ambao nao hawakupata ushindi wowote, baada ya kufungwa mechi mbili.

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuelekea mchezo huo, hawahitaji matokeo mengine zaidi ya ushindi pekee.

Ally alisema matokeo ya ushindi ndiyo yatakayofufua matumaini ya wao kufika hatua ya Robo Fainali ya Ligi Mabingwa Afrika.

Aliongeza kuwa, kabla ya kuanza safari ya kuelekea Morocco, viongozi walifanya kikao na wachezaji, benchi la ufundi na kusisitiza ushindi katika michezo iliyobakia kwa kuanza dhidi ya Wydad Casablanca.

“Tutakuwa ugenini kucheza dhidi ya Wydad Casablanca, ambao wamepoteza michezo yote miwili ya kwanza, hivyo tunaamini wataingia uwanjani kwa lengo moja la kupata ushindi wa kwanza kwetu.

“Hatutaki kuona likitokea kwetu, kwani sisi wenyewe pia tunautaka ushindi wa kwanza kwao, hivyo hatutaki matokeo yoyote katika mchezo huu zaidi ushindi, kwani sare na kufungwa kutaharibu mipango yetu ya msimu,” alisema Ally.

STORI NA WILBERT MOLANDI

MAMA LOVE KUNGWI -“NAISHI NYUMBA KODI YAKE MILIONI 6 kwa MWAKA -MIMI ni MAARUFU SANA WATU WANANIJUA”

Leave A Reply