The House of Favourite Newspapers

Simba Watinga Bungeni, Wapokelewa kwa Shangwe

KLABU ya Simba ambao ni Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL) mwaka 2017/18, leo Jumatatu, Mei 14, 2018 wametinga Bungeni jijini Dodoma baada ya kupata mwaliko wa Spika Job Ndugai.

Mwenyekiti wa Bunge, aliyekuwa akiongoza kikao cha leo, Najma Giga, Naibu Waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda ndiye alianzisha shangwe za kuwapokea Simba bungeni kabla hawajatambulishwa.

Kakunda kabla ya kujibu swali bungeni, alisema, leo ameamka saa 10 alfajiri akijiandaa kujibu maswali lakini furaha ya ubingwa wa Simba ilitawala kichwa chake hali ambayo ilipelekea wabunge wengine kushangilia.

“Sasa naamini Watanzania watapata wawakilishi wazuri wa michuano ya kimataifa, hawatatupa presha,” alisema Kakunda.

 

Mbunge wa Ilala, Dar es Salaam, Idd Azzan Zungu (CCM), alisema; “Humu ndani ya bunge kaingia mnyama mkali sana (Simba), lakini msihofu tuko salama,” wabunge wakaripuka shangwe tena.

Mbunge wa Mpwapwa (CCM), George Lubereje naye amewapongeza Simba akisema wamefanya kazi kubwa kuchukua ubingwa huo hata kabla ligi kumalizika.

Comments are closed.