The House of Favourite Newspapers

Simba Wazindua Kampeni Ya Ujenzi wa Uwanja Bunju – Video

0

UONGOZI wa Klabu ya Simba leo Desemba 17,2021 umezindua kampeni maalumu kwa ajili ya mashabiki,wanachama na wadau kuweza kuchanga fedha kwa ajili ya gharama za ujenzi wa kisasa.

 

Uwanja huo wa Mo Simba Arena gharama zake ambazo zinatarajiwa kutumika ni zaidi ya Bilioni 30 na wameweka wazi kwamba utakuwa ni mchakato endelevu na matumizi ya fedha yataendeshwa katika ukweli na uwazi.

 

Mtendaji Mkuu wa Simba,Barbra Gonzalez amesema kuwa kampeni hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuweza kufanikisha lengo hilo kubwa na nzuri kwa maendeleo ya timu hiyo.

 

“Tunamshukuru Rais wa Heshima, Mohamed Dewji kwa namna ambavyo ameweza kusema kuwa atatoa Bilioni mbili ambazo hizo zitaongezewa na zile zitakazochangwa kwa ajili ya kukamilisha mchakato wetu wa ujezi.

 

“Haina maana kwamba Simba hatuwezi hapana ila tumeamua kufanya hivi kwa kuwa Simba ni timu ya watu, timu ya wenye nchi mipango ilianza muda mrefu na Bodi imekaa na kuja na mpango mzuri wa namna ya kuweza kuchangia hizo fedha.

 

“Yote tunafanya kwa ajili ya maendeleo ya timu hii na tumekuja na kampeni inayokwenda kwa jina la ‘Tumeamua,tunaweza Simba yetu, Uwanja wetu’ hili ni jambo kubwa na tunafanya na wenye nchi na Simba ni timu ya watu,” amesema.

 

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema Uwanja huo wa Mo Simba Arena unatarajia kugharimu zaidi ya Bilioni 30.

 

“Jambo hili sio geni kwa sababu limeanza kutumika muda mrefu na hii sio harambee bali ni kwa ajili ya kuendeleza ule utamaduni wetu na umoja, makadirio ya uwanja huu ni takribani Bilioni 30,” amesema Mangungu.

Kutakuwa na namna tatu za kuchangia ambapo ni ile ya njia ya mtandao wa simu, lipa pesa pamoja na kulipa kwa kutumia benki.

 

Mangungu ameongeza pia wanafanya mawasiliano na benki nyingine pamoja na mitandao mingine ili kuweza kushirikiana nao katika suala hili.

Leave A Reply