The House of Favourite Newspapers

Wanajeshi 1000 Watimuliwa kwa Kukaidi Agizo la Chanjo

0

Zaidi ya Wanajeshi Wanamaji 100 wa Marekani wameondolewa jeshini kwa kukataa kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19 chini ya agizo la kiongozi wa nchi hiyo, Rais Joe Biden la kuhusu chanjo.

Idhaa ya Urusi, Russian Today imenukuu taarifa ya Marine Corps Times Ijumaa kuthibitisha kuwa hadi alhamis wanamaji 103 walikuwa wameathirika na uamuzi huo na walisubili kuondolewa kwa heshima ama kwa ujumla.

Msemaji wa Marine Corps Mej. Jim Stenger aliliambia jarida hilo kwamba misamaha 1,007 ya chanjo imekubaliwa kwa sababu za kiafya.

Maombi mengine 2,836 ya kusamehewa kwa sababu za kidini yamekataliwa hadi sasa. Kikosi hicho hakija toa msamaha wowote hadi sasa kwa misingi ya kidini juu ya chanjo ya UVIKO-19 ingawa kuna maombi 300 yaliyosalia.

Ingawa mwezi Novemba iliarifiwa kuwa Jeshi la Wanamaji lilikuwa na chanjo kidogo zaidi, idadi kubwa ya wafanyikazi wake – karibu asilimia 95 – wamepokea angalau dozi moja ya chanjo ya UVIKO-19. Wafanyakazi walikuwa wamepewa hadi Novemba 28 kupata chanjo dhidi ya virusi au kuomba msamaha.

Leave A Reply