The House of Favourite Newspapers

Simba: Wydad Wagumu, Lakini Hawatoki Kwa Mkapa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa

0

KUELEKEA mchezo wao wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kesho Jumamosi dhidi ya Wydad Casablanca, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally umekiri watakutana na timu ngumi lakini amechimba mkwara mzito kuwa Simba itashinda mchezo huo.

Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kweye Ligi ya Mabingwa Afrika, kesho Jumamosi wanatarajiwa kuwa wenyeji wa mabingwa watetezi wa mashindano hayo Wydad Casablanca kutokea Morocco, mchezo ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Simba wanaingia katika mchezo huo wakiwa na ari kubwa ya ushindi baada ya Jumapili iliyopita kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mtani wao Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Ni wazi tunatarajia mchezo mgumu sana kutokana na ubora wa wapinzani wetu, hii ni timu kubwa Afrika na ndio mabingwa watetezi hivyo ni wazi tunawaheshimu sana.

“Lakini ikumbukwe hapa wamekuja kwenye himaya yetu na kwenye kiwanja ambacho mengi ambayo yalikuwa yakioneaka hayawezekani yalifanikiwa, hivyo tumejipanga kuhakikisha Wydad hawatoki kwa Mkapa.”

Leave A Reply