Ajiua kwa kujipiga Risasi Mwanza
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mfanya biashara mmoja aliyejulikana kwa jina la Emmanuel Nyambera Mkazi wa Bwiru Msikitini Wilayani Ilemela jijini Mwanza amejiua kwa kujipiga Risasi kifuani kutokana na Migogoro ya kifamilia.
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema Tarehe 16.04.2023 muda wa saa 21:45 usiku, huko maeneo ya Bwiru Msikitini, kata ya Pasiansi, Tarafa na Wilaya ya Ilemela, kuliripotiwa taarifa ya Emmanuel Nyambera, miaka 40, mfanyabiahashara na mkazi wa Bwiru Msikitini aliyejipiga risasi kifuani upande wa kushoto na kupelekea kifo chake. Emmanuel Nyambera alikuwa akimiliki Bastola yenye namba za usajili TZCAR80190 Model namba 79 KCAL 38 aina ya charter ambayo inauwezo wa kuchukua risasi tisa (9) na ndio aliyotumia kujifyatulia risasi kifuani hali iliyopelekea kifo chake . Chanzo cha tukio hilo ni migogoro ya kifamilia iliyotokana na mgawanyo wa mali za familia ambapo Emmanuel Nyambera alikua hajalidhia jambo lililompelekea kuwa na msongo wa mawazo na kupelekea kujipiga risasi. Mwili wa Emmanuel umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi. Jeshi la Polisi Mkoa Wa Mwanza linaendelea kutoa wito kwa wananchi kutafuta njia nzuri na sahihi ya kutatua migogoro mbalimbali wanayokutana nayo ilikuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.