The House of Favourite Newspapers

Simba Yaiandalia Kipigo Yanga Uwanja wa Mkapa jijini Dar

0

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema wataingia kucheza Kariakoo Dabi kimkakati kuhakikisha wanashinda mchezo huo.

Dabi hiyo itakayowakutanisha Simba na Yanga, inatarajiwa kupigwa Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo huo, Simba itaingia vifua mbele ikiwa na rekodi ya kuifunga Yanga mabao 2-0 katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, huku pia ikishinda Ngao ya Jamii msimu huu kwa penalti.

Akizungumza na Spoti Xtra, Try Again alisema wanakwenda kucheza mchezo mwingine mgumu wa ligi dhidi ya Yanga wakitoka kuifunga Ihefu mabao 2-1.

Try Again alisema katika mchezo dhidi ya Ihefu, waliingia kucheza wakiwa na hofu ya majeruhi na kadi, lakini kuelekea Dabi wataingia kimkakati zaidi kwa lengo la kuwaondoa Yanga kileleni katika msimamo wa ligi.

“Mchezo wetu uliopita ulikuwa mgumu, lakini vijana wetu walijiandaa kupambana kuhakikisha tunapata pointi tatu, licha ya mbele kukabiliwa na mchezo mgumu wa dabi.

“Lakini pia tulicheza kimkakati kwa sababu tulikuwa tunakwenda kucheza mchezo mgumu wa dabi dhidi ya Yanga, hivyo hatukutumia nguvu kubwa.

“Kuelekea dabi hiyo, tutaingia kimkakati tena kuhakikisha tunapata ushindi, hiyo ni kutokana na ubora ambao wanao wapinzani, huku pia sisi tukiwa nao wa kutosha,” alisema Try Again.

STORI NA WILBERT MOLANDI

WAZIRI UMMY ANAWASILISHA MUSWAADA wa SHERIA ya BIMA ya AFYA KWA WOTE | DODOMA

Leave A Reply