Simba Yaichapa Bao 5-0 Majimaji FC katika FA

 

KLABU ya soka ya Simba kwenye mchezo wa kombe la FA jana, iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Majimaji ya Songea.

 

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, raia wa Ubelgiji, ilianza kwa kasi kipindi cha kwanza kwa kasi ambapo bao la kwanza lilifungwa na beki wa Simba Gadiel Michael dakika ya tatu baada ya Said Ndemla kupiga shuti kali lililogonga mwamba na kukutana na Gadiel ambaye alikuwa nahodha kwenye mchezo huo.

 

Mshambuliaji aliyeanza kikosi cha kwanza, Chris Mugalu, alipachika bao la pili dakika ya 16 lililowafanya waende kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa wameshinda mabao mawili.

 

Kipindi cha pili beki wa kati Ibrahim Ame alipachika bao la tatu dakika ya 78 na mshambuliaji namba moja wa Simba, Meddie Kagere, alipachika bao dakika ya 78.

 

Wakati Majimaji ambao walikuwa wakifanya mashambulizi kwa kumtumia Ismail Mussa wakiamini kwamba mchezo umekamilika, Luis Miquissone alifunga bao la tano dakika ya 88.

 

Ushindi huo unaifanya Simba kutinga hatua ya nne bora baada ya kuiondoa Majimaji leo ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

 

Sven amesema: “Sitaki kuskia wachezaji wangu wakikosolewa kwa kuwa wanafanya kazi kubwa kweli.”

 Tecno


Toa comment