The House of Favourite Newspapers

Simba Yaingia Anga Moja na Spurs, Inter Millan

0

KLABU ya Simba imeingia katika historia kubwa pamoja na klabu maarufu kubwa duniani kutokana na kuongoza kwa kufuatiliwa zaidi katika ukarasa wake wa Instagram kwa mwaka 2020.

 

Simba inaingia katika rekodi hiyo ikiwa ndio timu pekee kutoka barani Afrika huku ikiwa imezipita klabu nyingi kubwa na maarufu duniani.

 

Kupitia ukurasa rasmi wa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez aliposti picha ambayo ilionyesha kuwa timu hiyo ndio kinara kwa kufuatiliwa katika mtandao wa Instagram kwa mwaka 2020 duniani kote.

 

Simba imeingia katika rekodi hiyo ikiwa na wafuasi milioni 1.9 katika ukarasa wake wa Instagram huku ikiwa na wastani wa kukua kwa zaidi ya asilimia 89 jambo ambalo limefanya timu hiyo kuongoza duniani kote.

Nafasi ya pili ilikuwa ikishikiliwa na mtandao wa Transfermarket ambao una wafuasi milioni 3.9 huku ukiwa na wastani wa kukua kwa asilimia 79, nafasi ya tatu inashikiliwa na timu ya Bayer Leverkursen ya nchini Ujerumani ambao wana wafuasi 1.1 huku wakikua kwa asilimia 66.

 

Nafasi ya nne Inter Milan wenye wafuasi milioni 6.2 huku wakikua kwa asilimia 47, Sevilla wanashika nafasi ya 7 wakiwa na wafuasi milioni 1.1 wakikua kwa asilimia 41, Tottenham wanashika nafasi ya 8 wakiwa na wafuasi milioni 9.5 wakikua kwa asilimia 39.

Marco Mzumbe,Dar es Salaam

 

Leave A Reply