The House of Favourite Newspapers

SIMBA YAIPIGA BIASHARA UNITED 2-0, BOCCO ATUPIA

John Bocco

TIMU ya Simba leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo  wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Karume, Musoma. Mabao ya Simba yamefungwa na John Bocco dakika ya 33 na 40 kipindi cha pili.

 

Katika mchezo huo  kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima alitolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 75.

 

Baada ya kushinda Simba wamefikisha pointi 69 wakiwa nafasi ya pili wakiwa wamecheza michezo 27, Azam wako katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 66 kwa michezo 32. Nafasi ya kwanza inashikiriwa na timu ya Yanga ikiwa na pointi 74 wakiwa na michezo 32.

 

Aprili 29, mwaka huu timu ya Yanga itacheza na Azam FC katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 

 

Comments are closed.