The House of Favourite Newspapers

Simba Yairahisishia kazi Yanga CAF

SIMBA jana Jumatano ilishusha kipigo kingine cha mabao 4-1 dhidi ya Platinum Stars ya nchini hapa lakini Jumamosi itawafanyia Yanga kazi ya bure. Simba itacheza dhidi ya wapinzani wa Yanga kwenye michuano ya kimataifa, Township Rollers ya Botswana, Jumamosi mjini hapa.

 

Hiyo itakuwa ni nafasi adhimu kwa Yanga kusoma uimara na udhaifu wa wapinzani wao, ingawa hakuna taarifa rasmi kama Yanga watatuma mtu kwa vile Kocha Mwinyi Zahera anawasili Dar es Salaam leo Alhamisi.

Kwa sasa Simba na Township wapo kwenye maandalizi ya msimu mpya wa kimataifa mjini hapa sambamba na timu nyingine za Afrika.

 

Katika mchezo wa jana mchana dhidi Platinums Stars mabao ya Simba yalifungwa na kiungo mpya raia wa Sudan, Sharaf Shiboub kwa njia ya penati na Mzamiru Yassin pia alifunga moja.

 

Kiungo mahiri wa Zambia, Clatous Chama aling’ara baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo huo ulioshuhudiwa na Mtendaji Mkuu wa Simba, Cresentius Magori. Juzi Simba iliwafunga Orbret TVET mabao 4-0 na imesaliwa na mechi ya Township Rollers na Orlando Pirates.

Comments are closed.