The House of Favourite Newspapers

Simba, Yanga Zagawa Dozi Mapinduzi

0

SIMBA SC na Yanga SC, zimeanza michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kugawa dozi ya mabao 2-0
kila moja.
Katika mchezo wa kwanza, Simba iliifunga Selem View 2-0, huku Yanga ikipata ushindi kama
huo dhidi ya Taifa Jang’ombe.

 

Mechi zote zikichezwa kwenye Uwanja wa Aman, Zanzibar. Ilishuhudiwa Simba ikifunga mabao yake kupitia kwa Pape Sakho dakika ya 25 na Rally Bwalya dakika ya 53.

 

Kipindi cha kwanza Simba walikitawala sana ambapo wapinzani wao hawakufanikiwa kupiga hata shuti moja lililolenga lango.


Katika mchezo huo, Kocha
Mkuu wa Simba, Pablo Franco, aliwatumia baadhi ya wachezaji ambao hawana nafasi kubwa ya kucheza kikosi cha kwanza ambapo golini alianza Beno Kakolanya ambaye msimu huu hii ndiyo mechi yake ya kwanza ya kimashindano.


Wengine waliopata nafasi hiyo
ni Gadiel Michael na Jimmyson Mwanuke. Wachezaji waliopo kwenye majaribio katika kikosi cha Simba, Sharaf Shiboub na Cheick Ahmed Tenena Moukoro, walianzia benchi na kuingia kipindi cha pili. Shiboub alichukua nafasi ya Sadio Kanoute, huku Mzamiru Yassin akimpisha Moukoro.

Kiungo wa Simba, Rally Bwalya, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo na kukabidhiwa shilingi laki tano.

 

YANGA YAJIBU MAPIGO
Yanga ambao nayo iliibuka
na ushindi wa mabao 2-0 kwa kujibu mapigo ya Simba, ilitumia wachezaji wengi ambao nao hawana nafasi kikosini hapo msimu huu.


Pia iliwatumia wachezaji
wote iliowasajili kipindi hiki cha dirisha dogo ambao ni Aboutwalib Mshery, Salum
Abubakar ‘Sure Boy, Denis
Nkane na Chrispin Ngushi.

 

Nkane alianza vizuri kwa kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza akiwa na jezi ya Yanga ambapo alifunga bao hilo dakika ya 50.

 

Kabla ya bao hilo, Heritier Makambo, aliitanguliza Yanga kwa bao la kideoni dakika ya 33. Kesho Ijumaa, vigogo hao wa soka kutoka Tanzania Bara,watashuka tena dimbani hapo ambapo mechi ya mapema ni Yanga vs KMKM na Simba vs Mlandege.

STORI: KAZIJA THABIT | CHAMPIONI


Leave A Reply