Simba, Yanga Zawekewa Kamera

BODI ya Ligi iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetoa tahadhari kwa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ikiwemo Simba na Yanga kuwa makini katika mechi za mwisho na kusema kuwa inatuma watu maalumu kufuatilia mechi hizo ili kuepuka upangwaji wa matokeo.

 

Ligi inafikia tamati Mei 28 ambapo Simba imebakiza michezo mitano huku timu nyingine zikiwa zimebakiza michezo mitatu kukamilisha mzunguko wa ligi wa msimu wa 2018/19 ambapo hadi sasa bingwa bado hajajulikana.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mguto amesema kuwa, wanawatuma watu maalumu kufuatilia kila michezo inayochezwa kuanzia sasa ili kila timu ipate matokeo kulingana na jinsi inavyocheza.

 

“Suala la timu kulalamika lipo wazi hivyo tunahitaji kuwatuma watu maalumu kuweza kufuatilia mechi zitakazochezwa kwa kuwaongezea wale waliokuwepo ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa nakuepuka upangwaji wa matokeo.

 

“Vile vile mechi zote tutahakikisha zinaonyweshwa live ili kuona kila kitu kinachoendelea ili tupate kuona kila kitu kinachoendelea,” alisema Mguto ambaye ni kiongozi wa Coastal Union.

STORI NA KHADIJA MNGWAI, GPL

Loading...

Toa comment