The House of Favourite Newspapers

ads

Simba Yawakalisha Wajelajela Tanzania Prisons, Mkude Apeleka Kilio

0
Kiungo wa Simba Jonas Mkude akishangilia goli pekee kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya.

KLABU ya Simba leo Septemba 14, 2022  imefanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wajelajela Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

 

Bao pekee la Simba limewekwa kimiani na kiungo mkongwe Jonas Mkude baada ya kuunganisha pasi ya kichwa ilipigwa na Kibu Denis dakika ya 85 ya mchezo.

 

Kwa matokeo hayo Simba ambayo ipo chini ya Kocha mkuu wa muda Juma Mgunda imefikisha alama 10 sawa na mabingwa watetezi Yanga.

 

Leave A Reply