The House of Favourite Newspapers

Simeone: Tutamruhusu Griezmann Aondoke

Antoine Griezmann.

KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone amesisitiza kwamba klabu yake inaweza kumuuza staa wake, Antoine Griezmann kama walivy-ofanya kwa Diego Costa na Arda Turan.

 

Griez-mann, 26, anahu-sishwa na mipango ya kujiunga na Manchester United pia klabu nyingine kubwa za Ulaya zinatajwa kumuwania mshambuliaji huyo.

 

Lakini Griezmann raia wa Ufaransa aliyejiunga na Atletico mwaka 2014 akitokea Real Sociedad, ana mkataba na Atletico hadi Juni, 2022. Costa amerejea Atletico lakini Turan yupo Barcelona.

 

“Nawapenda wachezaji wangu na nataka kuona wanapiga hatua zaidi, mimi si mbinafsi kwao,” alisema Simeone na kuongeza;

“Endapo mchezaji ananifuata na kuniambia amepata nafasi ya kucheza mahali fulani, akiniambia hivyo kama alivyofanya Griezmann, nitamwambia hakuna tatizo. Najua anataka kukua zaidi.

 

“Kwa hiyo Griezmann ana nafasi ya kuondoka kwa mazingira fulani kama ilivyokuwa kwa Costa na Turan, maana tuliwaruhusu kuondoka.”

 

Griezmann amefunga mabao saba katika mechi 18 msimu huu na amefunga wastani wa mabao 25 katika misimu mitatu iliyopita.

MADRID, Hispania

Comments are closed.