The House of Favourite Newspapers

Simon Msuva Aipa Nafasi Yanga Kusonga Mbele

0

WINGA machachari wa Wydad Casablanca ya nchini Morocco, Simon Msuva, amesema licha ya Yanga kupoteza katika mchezo wake wa kwanza wakiwa nyumbani dhidi ya Rivers United, anaamini bado ina nafasi ya kusonga mbele katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga Septemba 12 walipoteza kwa bao 1-0 wakiwa nyumbani katika Uwanja wa Mkapa ambapo marudio ya mchezo huo ni keshokutwa Jumapili nchini Nigeria, Yanga wakiwa ugenini na wakitakiwa kushinda ili wasonge mbele.

Msuva kabla hajatimkia katika ligi ya Morocco alikuwa akicheza Yanga ambayo ilimuuza kwenda Difaa el Jadid ambako pia aliuzwa kwenda Wydad Casablanca.

Msuva alisema kuwa kupoteza kwa Yanga katika mchezo wa kwanza siyo kutolewa nje kwa timu hiyo huku akiamini kuwa kama Rivers waliweza kushinda ugenini pia Yanga wanaweza kuibuka na ushindi wakiwa ugenini, muhimu ni kujituma zaidi kwa wachezaji.

“Wachezaji wa Yanga wanatakiwa kutokukata tamaa na kujituma zaidi, kama ambavyo Rivers waliweza kupata ushindi na kufanikiwa ugenini, ambacho kinataikwa ni kuweka malengo ya kweli, naamini watafanikiwa kusonga mbele katika hatua inayofuata ya michuano hiyo.”

Leave A Reply