The House of Favourite Newspapers

Simulizi ya Denti Chuo Kikuu Kupooza

0

kupooza picha na global publishers (2) Mahmudu Said akiugulia.

Stori: MAYASA MARIWATA

MSOMI aliyehitimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),  Mahmudu Said (25),  amejikuta akikata tamaa ya kutimiza ndoto zake kimaisha baada ya kupooza sehemu ya mwili wake na kushindwa kupata jibu la kupona kwake, kutokana na kukosa fedha za matibabu.

Akizungumza kwa majonzi makubwa nyumbani kwao maeneo ya Yombo Dar, mwanafunzi huyo alisema, baada ya kuhitimu chuo kikuu mwaka jana na kutunukiwa shahada katika sanaa (BA -arts and Deveropment ) alianza kutafuta kazi lakini mwezi wa tatu mwaka huu ndipo alijikuta miguu ikikosa nguvu ghafla.

kupooza picha na global publishers (1)Akifafanua tatizo lake alianza kusimulia kwa kusema:

“Baada ya kumaliza chuo nilienda kupumzika Iringa kwa kuwa huko kuna watu wengi ninaofahamiana nao, sasa mwezi wa tatu nikiwa kwenye matumaini makubwa ya kupata kazi ndipo siku moja asubuhi nilipoamka nikaanza kuhisi viungo vyangu vya miguu na mikono havina nguvu.

“Niliipuuza hali hiyo nikaenda maskani ambapo kila baada ya muda hali ilizidi kuwa mbaya, nguvu kwenye magoti zikapotea na mkono wa kulia ukapoteza nguvu ukifuatiwa na wa kushoto, nikawa sijiwezi kwa chochote.

“Kutokana na hali hiyo ilinilazimu kwenda Hospitali ya Ipogoro ambapo nilichukuliwa vipimo vya damu lakini tatizo halikuonekana , ikabidi nije Dar na kwenda Hospitali ya Lupimo, nikaonekana mafuta yamesababisha mzunguko mbaya wa damu.

kupooza picha na global publishers (3)“Sikuweza kupingana nao, wakasema dawa ni shilingi laki nne lakini nikanunua nusu dozi kwanza ambapo niliitumia kwa siku nne nikaona hali yangu inazidi kuwa mbaya, ikabidi niende Hospitali ya Newala kwa ajili ya kufanyiwa mazoezi ya viungo napo ikashindikana nikapewa Rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Muhimbili nikapokelewa na kuambiwa nipimwe vipimo vya EMG na NCT, kwa kuwa mashine ya hospitalini hapo ilikuwa imeharibika ikamlazimu niende Hospitali ya PCMC ambapo vipimo niliambiwa ni shilingi laki tano.

“Pale walisema mishipa imetafunwa na wadudu waliosababishwa na ugonjwa wa Typhoid nilioumwa wiki moja kabla ya kupatwa na tatizo hilo, hivyo zinahitajika dawa za awamu mbili za kuua wadudu na kutibu ugonjwa, niliambiwa gharama ni shilingi milioni kumi na mimi familia yangu imeishiwa pesa,” alisema.

Akaongeza huku akilengwalengwa machozi: “Naomba Watanzania wenzangu wanisaidie.”

Aliyeguswa na tatizo la kijana huyu anaweza kuchangia gharama za matibabu kwa namba 0712 169814 na 0655 781899 au NMB ACC 21902400489.

Leave A Reply