The House of Favourite Newspapers

Siri Diamond Kununua Jumba la Kifahari Jirani na Zari Yafichuka

0
Diamond Platnumz; ni supastaa wa muziki nchini Tanzania.

Diamond Platnumz; ni supastaa wa muziki nchini Tanzania ambaye Oktoba 4, 2022, kwa mara ya kwanza alionesha jumba lake la kifahari lililopo nchini Afrika Kusini.

 

Diamond au Mondi ambaye ni mzaliwa wa Tandale jijini Dar, alionesha jumba hilo kubwa la kifahari lililopo jijini Johannesburg nchini humo.

 

Mbali na kuwa na vyumba vingi na samani za kupendeza, nyumba hiyo pia ina bwawa la kuogelea ndani yake.

“Ni vizuri sana kurudi nyumbani!” Alisema Diamond chini ya video iliyoonesha jumba hilo.

Katika video hiyo, baadhi ya washiriki wa timu yake ya muziki walionekana wakistarehe ndani ya jumba hilo katika vyumba tofauti vya kulala.

Diamond alitumia fursa hiyo kutangaza kuwa baada ya kupumzika nchini Afrika Kusini kwa muda wataendelea na ziara yao ya muziki katika mataifa mbalimbali.

 

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na ripoti kuwa Diamond mwenye umri wa miaka 32 anamiliki jumba la kifahari nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo, Diamond hakuwahi kuonesha jumba hilo kikamilifu hapo awali.

Mwanamama tajiri Afrika Mashariki na baby mama wa staa mkubwa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady.

Watu wa karibu wameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, kuna siri kubwa nyuma ya jumba hilo ambayo wengi hawaijui kuwa, Diamond amenunua jumba hilo jirani kabisa na nyumbani kwingine kwa baby mama wake, Zari The Boss Lady huko Johannesburg.

 

Inafahamika kwamba, Afrika Kusini ndiko anakoishi Zari pamoja na watoto wao wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan.

Zari ambaye ni raia wa Uganda amekuwa akiishi huko kwa miaka kadhaa ili kuweza kufuatlia biashara zake kwa karibu.

 

Watu wa karibu wa Diamond wanasema kuwa, Diamond aliamua kutafuta makao huko Afrika Kusini ili kupata fursa ya kuwa na kipindi kizuri pamoja na familia yake kila mara anapofanya ziara katika nchi hiyo.

 

Miezi kadhaa iliyopita, baba wa kambo wa Diamond, Uncle Shamte alifichua kuwa jamaa huyo amefanikiwa kununua viwanja 67 na kujenga majumba katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

 

“Nasibu ana nyumba nyingi. Nyumba kama 67. Mimi binafsi nina miaka mitano kwenye familia, sasa nasimamia nyumba ya 61. Hatujipi sifa kusimamia nyumba, lakini tunapozungumza sasa hivi hivyo ndivyo uwezo wake ulivyo,” alisema Uncle Shamte.

Stori; Mwandishi Wetu, Dar

Leave A Reply