The House of Favourite Newspapers

Siri Ya Robertinho Kwa Kibu Denis, Saido Yaanikwa Simba

0
Said Ntibazonkiza ‘Saido’

HATIMAYE siri ya Kocha Mkuu wa Simba, raia wa Brazil, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, kupenda kuwatumia wachezaji Kibu Denis pamoja na Said Ntibazonkiza ‘Saido’ ni kutokana na nyota hao kucheza kwa kufuata maelekezo yake bila hata kukosea.

Robertinho alijiunga na Simba Januari 3, mwaka huu akitokea Vipers SC ya Uganda, ambapo hadi sasa ameiwezesha Simba kumaliza ligi kuu ikiwa nafasi ya pili kwa msimu uliopita.

Kibu Denis

Chanzo chetu kutoka Simba kimeliambia Championi kuwa, ni vigumu sana kwa Kocha Robertinho kutowatumia Kibu na Saido wakiwa na utimamu wa kimwili kwani faida wanayompa ni kubwa sana.

 

“Kocha Robertinho, anapenda sana mchezaji anayeonyesha kupambana muda wote awapo uwanjani, hivyo siyo jambo rahisi kwake kwa sasa kuacha kuwapanga Kibu na Saido hata kama mashabiki hawaoni mchango wao.

“Kocha amekuwa akisema kila mara kuwa Kibu na Saido wanacheza kwa kufuata maelekezo yake yote hivyo anapenda kuwatumia kwa sababu hiyo, jambo ambalo si rahisi kwa kila mchezaji kupokea maelekezo ya kocha na kuyafanyia kazi bila hata kukosea,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

NA Musa Mateja, Gazeti la Championi

Leave A Reply