The House of Favourite Newspapers

SISTER FAY AWAKUMBUKA WATOTO YATIMA

Fay na timu yake wakiandaa vifaa vya kupikia.
…Akimwelekeza mmoja wa timu yake, Sad jinsi ya kutwanga vitunguu swaumu.
…Akiwapakulia watoto chakula.
…Akila chakula na watoto.
Timu Fay wakiwa katika picha ya pamoja na watoto pamoja na mmiliki wa kituo hicho.
Timu Fay wakiwa na mmiliki wa kituo, Kulthumu Yusuf aliyevaa ushungi (wa pili kushoto).

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Faidha Omary leo aliwakumbuka watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Al-Madina Children Home kilichopo Tandale jijini Dar akiwa na timu yake ambapo waliwapikia na kula nao chakula cha mchana.

 

Akizungumza na mwandishi wetu, Fay alisema ameamua kuwakumbuka watoto hao yatima wanaolelewa kituoni hapo kwani mastaa wengi wamekisahau na wanaenda kwenye vile vituo maarufu tu.

 

Aliendelea kusema kuwa kwa kile kidogo anachokipata ameamua kushiriki na watoto hao na anaamini Mungu atambariki na atakuwa anafanya hivyo kwa wiki mara moja.

 

“Nimeamua kuja kuwapikia hawa watoto, kula na kushinda nao siku nzima ya leo kwani unapokumbuka yatima na Mwenyezi Mungu anakuongezea riziki zaidi na zaidi,” alisema Fay.

 

Kwa upande wa mkurugenzi wa kituo hicho, Kulthumu Yusuf Juma alimshukuru Fay na timu yake kwa kuwatembelea katika kituo hicho chenye watoto 25, wamefurahi sana kwani amekuwa msanii wa kwanza kwenda na kupika pamoja na kula na watoto kwani wengine huwa wanaenda na vyakula vikiwa tayari au vikiwa havijapikwa na kuondoka.

 

“Mimi na watoto wangu tumefurahi sana kwa kweli maana Fay ndiye msanii wa kwanza kuna na chakula na kupika hapahapa, tunawaomba na wengine watukumbuke kwani tuna changamoto nyingi sana kama madaftari, unifomu, viatu, ada za watoto wanaofaulu kwenda sekondari kwani wengine wanashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa ada na mahitaji hayo mengine,” alisema Kulthum.

(Picha/habari: Gladness Mallya)

Comments are closed.