The House of Favourite Newspapers

Sistiinho: Sakata la Msuva na Wydad Casablanca Liwe Fundisho kwa Wachezaji Wazawa

0
Sistiinho mchambuzi wa soka kutoka kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa na Studio za Global TV na Global Radio

MCHAMBUZI wa soka kupitia kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa na Global TV na Global Radio amesema sakata la Kiungo mshambuliaji raia wa Tanzania Simon Msuva dhidi ya klabu yake ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco linapaswa kuwa fundisho kwa wachezaji wazawa juu ya kujua umuhimu wa haki katika mikataba yao.

 

Msuva aliishitaki Klabu yake ya Wydad Casablanca kwa Shirikisho la Soka Duniani FIFA kutokana na kushindwa kumlipa pesa zake za misharaha pamoja na pesa ya ada ya usajili ambapo jana FIFA ilitoa maamuzi kwa Wydad kumlipa Msuva kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 za kitanzania ikiwa ni ada ya uhamisho wake pamoja na malimbikizo ya mishahara.

Sistiinho amesema sakata la Msuva linapaswa kuwa fundisho kwa wachezaji wazawa

Kupitia kipindi cha Krosi Dongo Sistiinho amenukuliwa akisema:

“Mi nafikiri ni funzo kwa wachezaji wetu wa ndani unajua tumeona wachezaji wengi wa ndani mara ya mwisho sikumbuki nilisikia lini kesi kati ya mchezaji na viongozi kwenye masuala ya mikataba na wachezaji wamekuwa wakionewa sana, nafikiri hili la Msuva linaonesha funzo, Msuva alikuwa kimya sana hapa katikati kipindi hiyo kesi inafanyiwa kazi huko CAS sasa hii itaongeza chachu kwa wachezaji kupambania maslahi yao.”

FIFA imeiamuru Wydad Casablanca kumlipa Msuva kiasi cha Shilingi Bilioni 1.6 za Kitanzania

Aidha kumekuwa na stori zinazomhusisha mchezaji huyo kumalizana na klabu yake ya zamani ya Yanga kuhusu kuitumikia kwa msimu ujao, kwa muda mrefu Msuva amekuwa hana timu kufuatia kuachana na miamba hiyo ya soka barani Afrika ambao kwa sasa ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Leave A Reply