The House of Favourite Newspapers

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (13)

sitasahau

 

ILIPOISHIA

“Unamfahamu mzee mmoja anaitwa Samike? Ana nywele nyeupe, nyus…” kabla sijamaliza kuzungumza, kijana alibadilika na kuwa yule mtu wa ajabu aliyekuwa akinifukuza. Nikaanza kukimbia.

 

ENDELEA KUISOMA…

Nilikimbia kufuata barabara niliyokuja nayo. Naye alinikimbiza. Kama kawaida alishika upanga. Niliutazama kwa jicho la kuibia, tofauti na siku zote safari hii upanga ulisafishwa, ukanolewa vyema na ulikuwa na makali kuwili. Nilikimbia kuyanusuru maisha yangu.

 

Watu walinishangaa kwa jinsi nilivyokimbia. Mtu yule wa ajabu niliweza kumwona mimi pekee. Wao hawakumwona. Wapo waliosikika wakinibeza: “Unafanya mazoezi mchana wote huu!” wengine walizomea: “Huyoo! Kafumaniwaaaah,” hawakukosea, walikuwa sahihi. Ni kweli nilifumaniwa. Nilifumaniwa na kifo.

 

Nilipita Kamara nikikimbia kama bodaboda. ‘Rafiki’ mwenye upanga aliendelea kunifukuza. Nililoa jasho chapachapa. Sikujali, nilitambua jasho la mtu haliendi bure. Nikachanganya miguu. Mbio tu.

nikiendelea kukimbia, aliyenikimbiza alianza kutoa miungurumo ya kutisha. Nikajua leo nimekwisha… sitasahau…BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Comments are closed.