The House of Favourite Newspapers
gunners X

Siwema Afungukia Kumuona Mwanaye kwa Nay

Nay wa Mitego akiwa na watoto wake.

MZAZI mweza wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Siwema Edson amefungukia ishu ya kumuona mwanaye, Cartes kuwa, si kweli kwamba hajawahi kumuona tangu aondoke kwa jamaa huyo.

 

Siwema mwenye maskani yake jijini Mwanza aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, si kweli kwamba hajawahi kuomuona mtoto wake kwani mara nyingi anapokwenda kumuona kwa mama wa mwanamuziki huyo, Nay anakuwa hajui.

 

“Naongea naye kila mara, nimeshakwenda kumuona zaidi ya mara tatu, sema tu baba yake hajui hivyo angekuwa anamuuliza mama yake angempa jibu,” alisema Siwema.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.