The House of Favourite Newspapers

Skendo Ya Kubadili Wanaume…Wolper Amekoma!

 

Jacqueline Wolper akicheza na Barnaba.

DAR ES SALAAM: Muigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amemwagana na mpenzi wake, Barnaba Shelukindo ‘Brown’ na kusema amekoma kuingia kwenye uhusiano na wanaume wenye kiburi na wasiopenda kujishusha hivyo kwa sasa anabaki mwenyewe.

 

Kufuatia muigizaji huyo kushindwa kudumu kwenye uhusiano na wanaume tofauti huku wakidaiwa kumkimbia, Risasi Jumamosi limepenyezewa sababu tano zinazotajwa kuwa ndio chanzo cha mrembo huyo kuachwa kwenye mataa na wanaume.

Wolper akiwa na mpenzi wake Brown.

Akizungumza na mwanahabari wetu, shosti wa karibu na muigizaji huyo aliyeomba hifadhi ya jina, alisema kila mwanaume aliyewahi kuwa na Wolper kisha kumwagana naye ana sababu zake lakini zipo sababu tano za jumla zinazomfanya mrembo huyo aachwe na wanaume.

 

“Kila mmoja atakuwa alimuacha kwa sababu zake lakini kiukweli zipo sababu za jumla ambazo mimi kwa kuwa ni mtu wangu wa karibu, naamini kabisa zimechangia kwa kiasi kikubwa, wanaume kushika njia na kumuacha Wolper,” alisema shosti huyo.

 

Rafiki huyo alizitaja sababu hizo kama ifuatavyo:

SABABU YA KWANZA

“Unajua Wolper ana mapenzi ya dhati. Anataka akiwa na mwanaume awe yeye peke yake. Anapogundua tu kuna mwanamke mwingine anafaidi penzi lake huwa hapo hapo anakata uhusiano kama vile kuzima swichi ya taa.

 

SABABU YA PILI

“Unywaji wa mitungi nao umechangia kwa kiasi kikubwa wanaume kummwaga Wolper. Wanaume wengi aliokutana nao sio wanywaji sasa wanashindwa kubeba udhaifu huo, wanasepa.

 

SABABU YA TATU

“Sababu ya tatu ninayoiona kwa shoga yangu ni mchapakazi. Wananaume wengi waliomkimbia, walikuwa hawapendi zile harakati zake za kila siku, mara dukani mara wapi, wamejikuta wakijiondo

wenyewe kwa kudhani wanasalitiwa.

 

SABABU YA NNE

“Japo ni shoga yangu lakini ukweli ni kwamba Wolper anapenda kuwa juu sana kwa wanaume. Hiyo imemponza sana kwa wanaume. Si unajua wanaume hawapendi kuwa chini, wakiona hivyo tu, wanasepa.

 

SABABU YA TANO

“Safari za nje ya nchi pia ni sababu kubwa iliyomfanya Wolper aachwe na wanaume wengi. Si unajua wivu tena. Wanashindwa kuelewa kwamba safari zake za nje ya nchi mara nyingi ni za kibiashara, wao wanaamua kusepa zao,” alimaliza rafiki huyo.

 

Katika mazungumzo yake kuhusu masuala ya uhusiano na jinsi alivyoachana na wanaume tofauti, Wolper alianza kwa kumzungumzia mpenzi wake wa hivi karibuni.

Alisema alimuweka wazi mpenzi wake Brown akijua wazi ni mtu ambaye angeweza kudumu naye kwa muda mrefu kwa kuwa alimuona ni mtu muelewa lakini wameshindwa kuendelea na safari yao kutokana na tofauti za hapa na pale.

 

Wolper alisema kuwa ameamua kubwaga manyanga kwa mpenzi wake huyo si kwamba ni muhuni au hajui kupenda lakini ni mtu ambaye ana kiburi na wala hawezi kuomba sahamani pindi anapokosea.

 

“Siwezi kusema Brown hakuwa na mapenzi ya dhati kwangu au alikuwa na wanawake wengine kitu kilichokuwa kikiniudhi ni kwamba hajui kuomba msamaha pale anapogundua amekosea na ni mtu mwenye kiburi sana, nimekoma kwa kweli nimeamua kukaa peke yangu,” alisema Wolper.

 

Alipoulizwa kuhusu sababu hizo tano zilizotajwa na shosti yake, Wolper hakutaka kueleza kwa undani akidai kuwa ni mtazamo ambao kila mtu anaweza kusema lake lakini ukweli anaujua yeye mwenyewe.

 

Mbali na Brown, Wolper amewahi kuwa na uhusiano na staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’, Mkongo Rajab Mwami, mfanyabiashara Ramadhan Mtoro ‘Dallas’, Mkongo na G. Modo ambao wote kwa sasa wamechukua hamsini zao.

 

 

 

 

Comments are closed.