The House of Favourite Newspapers

Smartlab Limited Na Ndaki Ya Habari, Mawasiliano Na Teknolojia (COICT) Wasaini Makubaliano Ya Kukuza Uvumbuzi Na Ujasiriamali

0
Dk. Dr. Mercy Mbise, Kaimu Rasi, Ndaki ya Habari, Mawasiliano, na Teknolojia.

Kampuni ya Smartlab Limited, na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ndaki ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia, watangaza ushirikiano wao mpya katika kukuza uvumbuzi na ujasiriamali nchini Tanzania.

Smartlab Limited, kampuni iliyojikita kwenye uvumbuzi  na mafunzo ya kiteknolojia, imakua mstari wa mbele kutengeneza majukwaa yanayowapa vijana ujuzi, fursa na mitaji ili kutengeneza jamii inayoenda na kasi ya teknolojia.

Ushirikiano huo utawezesha Smartlab Limited, kitengo cha uvumbuzi chini ya kampuni mama Smart Africa Group, kuchangia utaalamu na rasilimali zake kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kushirikiana na kuendeleza miradi ya kiteknolojia.

Bw. Larry Ayo, Mkurugenzi wa Biashara Smartlab Limited

Ushirikiano huo pia utasaidia kuziba pengo kati ya wasomi na tasnia, kuhakikisha wahitimu wanaujuzi muhimu ili kuendana na soko la ajira.

“Tunajivunia kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ndaki ya Habari, Mawasiliano, na Teknolojia kukuza miradi na program za uvumbuzi nchini,” alisema Bw. Larry Ayo, Mkurugenzi wa Biashara Smartlab Limited. “Ushirikiano huu utasaidia kuwapa kizazi kijacho cha wataalamu wa teknolojia ujuzi wanaohitaji ili kufanikiwa katika sekta hii, na tunajivunia kuwa sehemu ya mpango huu.”

Ushirikiano huu utahusishwa kwenye miradi ya utafiti, ubadilishanaji wa maarifa, na uundaji wa miradi ya uvumbuzi inayoendana na mahitaji ya sasa kwenye soko la ajira.

Mkurugenzi Mtendaji wa Smart Group Africa, Edwin Bruno akizungumza na vyombo vya habari baada ya kulitiliana saini makubaliano hayo.

Ushirikiano huo pia utawapa wanafunzi fursa zingine nyingi kama mafunzo kwa vitendo, ushauri, na miongozo itakayowapa uelewa na uzoefu wa tasnia tofautitofauti.

“Tunafuraha kushirikiana na Smartlab Limited katika mpango huu muhimu,” alisema Dk. Dr. Mercy Mbise, Kaimu Rasi, Ndaki ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia.

Dr. Mbise na Larry wakionesha mikataba hiyo baada ya kusainishana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Smart Group Africa, Edwin Bruno na kushoto ni Mratibu wa Ubunifu Dr. Moses Ismail ambao nao walishiriki kwenye tukio hilo.

“Ushirikiano huu unaendana na dhamira yetu ya kutoa elimu inayofaa na yenye ubora wa juu ambayo inawatayarisha wanafunzi wetu kwa taaluma zenye mafanikio katika tasnia ya teknolojia.”

Kutiwa saini kwa ushirikiano huu ni hatua muhimu. Sio tu katika juhudi za kuendeleza ubunifu na teknolojia lakini pia kukuza uvumbuzi, ujasiriamali, na uchumi wa Tanzania kwaujumla

Leave A Reply