The House of Favourite Newspapers

SNURA AFUNGUKIA KUPEWA MIMBA NA BEN’TEN

UNAPOTAJA wasanii warembo wanaofanya vizuri Bongo Flevani, huwezi kuacha kulitaja jina la Snura Mushi ‘Snuu Sex’. Amelisumbua anga la Bongo Fleva kwa ngoma kali ikiwemo Majanga, Chura na Shoga Yake Mama.

Star Showbiz imefanya naye mahojiano ndani ya Studio za Global TV, karibu umsikilize:

Star Showbiz: Snura labda moja kwa moja tuanze na muziki wako, kwa nini nyimbo zako ‘zina-base’ sana uswahilini?

SNURA: Kwanza kabisa watu wanatakiwa wajue kwamba mimi ni msanii ambaye nimetokea kwenye maisha ya uswahilini, kwa hiyo ndio maana nyimbo zangu nyingi ni za uswahilini hata ukiangalia ngoma yangu ya kwanza (Majanga) inazungumzia maisha yangu ya uswahilini, lakini mbali na hivyo nilishawahi kujaribu kufanya ngoma za kishua kama vile Moyo Niache niliofanya na Aslay lakini haikutoboa nikaambulia patupu.

Star Showbiz: Idea ya kutoa Wimbo wa Vumbi la Mguu uliitoa wapi?

SNURA: Vumbi la Mguu ni maisha yangu halisi niliyoyapitia, ni wimbo ambao naupenda kwa sababu unaelezea uhalisia wa maisha yangu.

Star Showbiz: Kuna kipindi ulichora ‘tattoo’ ya piko kwenye kifua chako na kuandika jina la mpenzi wako Minucalipto, kwa nini uliamua kuchora ya piko na sio ya kudumu?

SNURA: Unajua mimi ni mtoto wa Kiislamu kuna vitu siwezi kupitiliza, itanigharimu baadaye ndio maana mambo ya kuchora tattoo na mimi ni vitu viwili tofauti kwa sababu pia siamini kama nitaishi maisha haya siku zote. Haya maisha ni ya muda tu, kuna muda utafika nitaishi maisha mengine nitajutia vitu kama hivyo nikishavifanya. Ndiyo maana ninaiangalia sana kesho, sitazami leo tu!

Star Showbiz: Kwa hiyo hutegemei kabisa kuchora tattoo ya kudumu ya mwanaume kwenye mwili wako?

SNURA: Siwezi kuja kufanya kitu kama hicho ila nikijisikia ndio kama hivyo, naenda nachora tu tattoo ya piko basi lakini siwezi kujichora tattoo kwenye mwili wangu. Hicho kitu hakiwezi kutokea kabisa kwenye maisha yangu.

Star Showbiz: Unajisikiaje unapoambiwa unatoka na kibenten (Minu)?

SNURA: Mimi mwenyewe huwa nashangaaga watu wanadai eti natoka na kibenten, kwa sababu mimi sio mtu wa kwanza kufanya hivyo hata mtume wangu Mohammed (SW) alizidiwa umri na mkewe. Alimzidi karibia miaka 15 kwa hiyo hilo suala sio mimi wa kwanza kulianzisha sisi wenyewe tumelikuta kwa hiyo sio kitu cha ajabu.

Star Showbiz: Kuna kipindi mpenzi wako Minucalipto aliposti picha yako kwenye akaunti yake na kuandika kwamba una mimba, ni kweli?

SNURA: (Anacheka) tusubiri tu muda utafika tutaiona kama kweli ipo au haipo, maana mimba huwa hazijifichi itajulikana tu.

Star Showbiz: Mna mpango wa kufunga ndoa?

SNURA: Bado, yani niseme kwa kifupi tu kuhusu ndoa Mwenyezi Mungu ndiyo anajua kwa hiyo tusubirie tuone. Binafsi siwezi kusema lolote.

Star Showbiz: Inafahamika kwamba mpenzi uliyenaye sasa hivi ulimuiba kwa Nisha, unaweza kutuambia uhusiano wako na Nisha sasa hivi ukoje?

SNURA: (Anacheka) Sikumuiba mpenzi wangu kwa Nisha, kwanza namuiba vipi yani kwa sababu yule mwanaume sio mtoto mdogo kwamba naweza nikamuiba. Aliridhishwa na mimi ndiyo maana akanifuata na kuhusu Nisha tupo vizuri tu, hatuna tatizo lolote maana hata kwenye kazi huwa tunasapotiana.

Star Showbiz: Asante sana kwa muda wako!

SNURA: Asante na wewe pia.

MEMORISE RICHARD

Comments are closed.