The House of Favourite Newspapers

Snura atoboa siri ugomvi na Shilole

0

MWANAMAMA anayefanya vizuri kunako muziki wa Singeli Bongo, Snura Mushi ametoboa siri ya ugomvi wake na msanii mwenzake, Zuwena Mohammed au Shilole kuwa chanzo cha yote ni wimbo wake wa Majanga.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na +255Global Radio jana, Alhamisi, Snura au Mamaa Majanga alisema kuwa, hapo ndipo tatizo lilipoanzia na hadi sasa hali si shwari.

“Ni kweli hatuna uhusiano mzuri na hatujawahi kuwa marafiki tangu tuzaliwe, hatujawahi kukaa na kupiga stori.

“Kilichoniponza ni Majanga, wote tulikuwa kwenye Bongo Movies, lakini kila mtu alikuwa anatamani kuingia kwenye muziki. Yeye ndiye aliyeanza kufanya wimbo na Q Chief.

“Nilipotoa wimbo wangu wa Majanga ukakubalika na watu wakaanza kusema najua kuimba na ngoma ya Majanga ikawa kubwa mno na kufunika mpaka wakubwa.

“Sasa watu wakaanza kumuambia amekuja kuzuga tu kwenye muziki na haniwezi kwa sababu mimi nilitoka mwenyewe, lakini yeye alibebwa na Q Chief.

“Cha msingi kuliko kuangalia watu wanasema nini, cha kumfanya ni kutoa ngoma kali na kuacha watu waseme kwa sababu yeye (Shilole) hakufurahia kusikia maneno ya watu kwamba nimemfunika ndipo akaanza kuniandama, lakini hakuna kingine zaidi ya hilo,” alisema Snura ambaye ameachia EP yake inayokwenda kwa jina la Jini.

STORI; KHADIJA BAKARI, DAR

Leave A Reply